Ni
jambo la kushangaza na ni vigumu kukuta viongozi wa kanisa wakiwatoza
waumini wao ada ili waweze kuhudhuria huduma ya neno la Mungu.
Lakini hii imetokea kwa waumini wa kanisa la Christ Embassy ambao
wameonekana kutokua na furaha baada ya kutakiwa kulipa 1000 Naira
ambayo ni fedha ya Nigeria kama kiingilio katika mkesha wa mwaka mpya
ulioandaliwa na Mchungaji Chris Oyakhilome.
Chanzo hicho kilisema sera hiyo ya
kulipa kiingilio ndani ya kanisa hilo siyo mpya na ilishawahi kufanyika
kwa mara nyingine mwaka mpya 2010 ingawa wengi hawakupendezwa na tukio
hilo.

Hii imeonekana kama ubaguzi kwa wasio nacho na uongozi wa kanisa ulisema umeamua kufanya hivyo ili kupunguza wingi wa watu wakati wa mkesha wa kuupokea mwaka mpya.
“Kanisa lina uwezo wa kubeba waumini 20,000 na limeweza kutengeneza zaidi ya Naira milioni 20 kutokana na mauzo ya tiketi za kuingia kanisani kupata huduma hiyo”kiliongeza chanzo hicho cha habari.
