
Programu ya simu ya mkononi kuhusu taarifa za Ebola huenda ikawa suluhu
Wakati
ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuwa tishio katika baadhi ya nchi Afrika
magharibi, Wataalam wa afya nao wameendelea kuweka jitihada zaidi
kuhakikisha kuwa wanaumaliza ugonjwa huo.
Katika jitihada zao hivi
sasa wamebuni mpango wa mawasiliano ya simu ya mkononi wenye programu
maalum inayotoa taarifa kutoka maeneo yaliyokumbwa na Ebola.Programu hii ya simu imesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini Guinea ambapo ugonjwa huu umesambaa kwa kiasi kikubwa, programu hii huweza kuonesha maeneo ambayo yako hatarini kuathiriwa naVirusi vya Ebola.
Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu duniani, UNFPA linatoa elimu kwa wafanyakazi wa jumuia kuhusu namna ya kutumia programu hiyo inayowezesha kushirikisha taarifa kwa kwa wataalamu wa afya katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.