
Mchezaji
mkongwe wa Arsenal Thierry Henry amefichua kuwa ndoto yake kuu ni
kumrithi Mkufunzi Arsene Wenger katika kilabu ya Arsenal.
Mchezaji
huyo wa zamani ambaye ndio anayeongoza kwa idadi ya mabao katika kilabu
hiyo akiwa na magoli 228 aliripotiwa kupewa fursa ya kuanza kufunza
soka katika chuo cha ukufunzi wa soka katika kilabu hiyo mapema mwezi
huu.Raia huyo wa Ufaransa amekiri kwamba ana mipango ya kumrithi Wenger wakati kocha huyo atakapoamua kustaafu.
Akizungumza wakati wa maonyesho ya Jonathan Ross Show,Henry alisema:

Lakini ni sharti niwe na uzoefu wa kutosha kuchukua wadhfa huo.
Kuwa Mkufunzi wa Arsenal ni ndoto yangu kubwa ,lakini nafaa kujifunza mwanzo ,hicho ndicho kitu muhimu''.