
Mmoja wa wanasiasa maarufu wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov
ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.
Mwanasiasa huyo alipigwa risasi nne kutoka nyuma na watu waliokuwa ndani ya gari alipokuwa akitembea nje ya makao makuu ya serikali.
Bwana Nemtsov ambaye alihudumu kama naibu waziri mkuu wakati wa uongozi wa rais Boris Yeltsin alikuwa akimshutumu vikali rais Vladimir Putin.

Kwenye mahojiano mapema mwezi huu bwana Nemtsov alisema kuwa alikuwa na hofu kuwa rais Putin angemuua.