IKULU YA RAIS YASHAMBULIWA SOMALIA.

By | 05:25
                     
Alshabaab
Washukiwa kadhaa na wapiganaji wa Kisomali, wamerusha makombora hadi katika ikulu ya Rais katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Wakuu wa usalama wanasema kuwa mlinzi mmoja ameuawa katika shambulio hilo.

Kundi la wapiganaji wa Al-Shabab limeshambulia mara kadhaa mji huo mkuu kwa mabomu, likijaribu kupindua serikali ya taifa hilo inayoungwa mkono na mataifa mbalimbali duniani.
Ijumaa iliyopita, walipuaji wa kujitolea muhanga waliwaua zaidi ya watu 20 walipolenga mgahawa maarufu mjini Mogadishu Central Hotel ulioko karibu na ikulu ya Rais.
Newer Post Older Post Home