
Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amehoji kuhusu shutuma za Waziri
Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu msimamo wake kuhusu Mpango wa
Nuklia wa Iran.
Netanyahu amekosoa Marekani na nchi nyingine za
magharibi kwa kile alichokiita ''kushindwa'' kuizuia Iran kutengeneza
silaha za nuklia.Kerry amekosoa Shutuma za Netanyahu alipokuwa akijibu tamko lililotolewa dhidi ya Marekani na nchi za magharibi kuwa ''zimekubali hali halisi kuwa Iran itakuwa na uwezo wa kutengeneza malighafi za kutengeneza silaha za Nuklia miaka michache ijayo''