MTANGAZAJI wa
Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka
kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir
(CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au
amuombe radhi kupitia kipindi chake.
Akiongea na Uwazi, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa
mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea
mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika
kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.
Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye
aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye
alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema
Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza
mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa
Deusi.
