Kinondoni Dar, ishu ni kesi ambayo tayari imefika kituo cha
Polisi Oysterbay ambapo mwenye nyumba mmoja amekuwa akichukua kodi kwa
wapangaji wengi ambao wanaletwa kwa nyakati tofauti halafu anawadanganya
kwamba kuna watu wanakaribia kuhama vyumba vitakuwepo kitu ambacho sio
kweli.
Baada ya wapangaji hao kushtuka kwamba
wanafanyiwa utapeli mmoja wao alimkamata mwenye nyumba huyo na kumpeleka
Kituoni hapo, amekaa kwa zaidi ya wiki moja huku wakipewa taarifa na
askari kwamba madeni ya wapangaji hao inakaribia milioni 40 na mwenye
nyumba huyo hana hela kuwalipa wote wanaomdai.

Picha hii imewekwa na Geah Habib katika ukurasa wake Instagram, kinachoonekana hapo ni ‘mwenye nyumba’ huyo, nyumba yake na mkataba wa mpangaji mmoja aliyetapeliwa.