WAZAZI HAWAKUPENDEZWA NA UHUSIANO WA MTOTO NA MPENZI WAKE,WAKAAMUA HIVI.

By | 00:24
girl
Siku za nyuma kulikuwa na story ambazo tuliwahi kuzisikia ama watu wazima
wanaweza kukumbuka enzi hizo wazazi wanakuchambulia mchumba au mpenzi
wa kuoa ama kuolewa, hii siku hizi inaonekana kuwa imepungua kwa kiasi kikubwa,
kumbe sio sisi peke yetu wenye tuliowahi kuwa na utamaduni huu.

Story inatoka China, msichana Zhang Qi ambaye ana miaka 24 amekuwa akiishi 
kwa kunyanyaswa na familia yake tangu mwaka 2009 ambapo alifungiwa ndani ya 
chumba na wazazi wake ambao waliamua hivyo kutokana na kutopendezwa 
na mtoto wao kuwa na uhusiano na kijana wa kiume ambaye wao hawakupendezwa naye.
PAY-Zhang-Qi
Hii ndio nyumba aliyofungiwa msichana huyo kwa miaka sita.
Wazazi walifanya maamuzi hayo magumu kama njia ya kuwatenganisha huku
 wakiwadanganya majirani kwamba msichana huyo ana matatizo ya akili ndio  
maana wameamua kumfungia ndani muda wote na kumhudumia kila kitu ndani 
ya chumba kwa muda wote huo.
PAY-Zhang-Qi (1)habgf
Picha zikionesha nje na ndani ya chumba alichofungiwa Zhang
Majirani wanasema wazazi wake ni wakali na hawakutaka jirani yoyote kujihusisha 
na ishu ya msichana huyo hivyo ikawa ngumu kujua kama ni kweli ana matatizo ya akili au hapana.
Polisi wanafanya upelelezi juu ya tukio hilo huku msichana huyo pia akifanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Newer Post Older Post Home