
Arsenal hoi dhidi ya Monaco UEFA
Matumaini
ya Arsenal kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo
imeingia nyongo hapo jana baada ya kukubali kipigo nyumbani mbele ya
mashabiki wao kutoka kwa Monaco ya Ufaransa cha mabao matatu kwa moja.
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Dimitar Berbatov ambaye naye alirejea England alikuwa ni miongoni mwa waliopachika magoli hayo kwa upande wa Monaco.
Huku magoli mengine yakipachikwa na Geoffrey Kondogbia na Yannick Ferreira Carrasco.
Goli la kufutia machozi la Arsenal limefungwa na Oxlade Chamberlain.