BAYERN MUNICH NAYO YAJITOSA KUNASA SAINI YA DI MARIA.

By | 04:05
                diiii
Klabu za ligi kuu ya England zipo katika maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu huku baadhi ya klabu zikianza mchakato wa kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya kutumikia klabu zao.
Wakati winga wa Manchester Angel Di Maria akiendelea kuwa gumzo kutokana na dalili za klabu yake ya Manchester kutaka kumtema, Bayern Munich imeanza mikakati ya kutaka kumsajili ili aitumikie msimu ujao.
Di Maria bado ana mkataba na klabu yake ya Manchester na huenda klabu hiyo ikamtoa kwa mkopo kwenda kucheza kwenye klabu yoyote inayomtaka.
Bayern imesema ipo tayari kutoa ofa kubwa zaidi ya iliyotangazwa na Paris St Germain ambayo nayo imepania kumnyakua winga guyo raia wa Argentina.
Newer Post Older Post Home