Waziri
mkuu wa Uingereza aliyechaguliwa kwa awamu ya pili David Cameron
anatumia wikendi hii kukamilisha orodha yake ya mawaziri baada ya chama
chake kushinda kwa uchaguzi mkuu nchini Uingereza.
Cameron tayari amemchagua Goerge Osborne ambaye tayari amefanywa kuwa waziri wa kwanza wa maswala ya kitaifa.
Wakati huohuo Vyama vya leba na Liberal Democrats vimeanza kuwatafuta viongozi wapya.

Ed Miliband na Nick Clegg walijiuzulu siku ya Ijumaa,pamoja na Kiongozi wa chama cha UKIP Nigel farage kufuatia matokeo mabaya na kuviwacha vyama vyao vikimtafuta kiongozi wa upinzani anayeweza kuuongoza upinzani kuunda serikali mpya.
BBC SWAHILI.