
Ukiizungumzia Chelsea kwa sasa ndio klabu bora kwenye ligi kuu ya England baada ya kutwaa kombe hilo msimu huu nakutangazwa kuwa machampion wapya.
Pamoja na Chelsea kuonekana ni bora lakini kwa upande wa kocha wao Jose Mourihno bahati haikuwa
yake kwa mara ya pili tena baada ya kushindwa kushinda nafasi ya meneja bora wa mwezi April msimu huu.
Mourihno akiwa katika moja ya mechi za ligi kuu
Badala yake kocha wa klabu ya Leicester, Nigel Pearson amechaguliwa kuwa meneja bora kwa mwezi wa nne.
Mourihno pia
msimu wa 2005/6 baada ya kutwaa ubingwa hakuweza kushinda nafasi hiyo na
sasa anasubiri kama ataweza kushinda kocha bora wa mwaka mwezi huu
baada ya ligi kumalizika.