MADRID KUFUKUZA KOCHA?

By | 04:42






                          carlo-ancelotti_z7b64u1sridq16bt29nnx3n9o

Baada ya kukamilisha msimu ambao klabu ya Real Madrid imekosa kutwaa taji lolote , uongozi wa klabu hiyo uko tayari kumfukuza kazi kocha wa timu hiyo Mtaliano Carlo Ancelotti huku orodha ya warithi ikiwa imeandaliwa .
Ripoti kadhaa nchini Hispania zimedai kuwa rais wa klabu hiyo Florentino Perez tayari amefikia uamuzi wa kumfukuza kazi kocha huyo na zimebaki saa chache kuanzia sasa ambapo kocha huyo ataonyeshwa mlango wa kutokea .
Ancelotti mwenyewe bado hajaarifiwa juu ya mpango wa kumfuta kazi ambao rais wa Real amekuwa nao kichwani kwake kwani ana mkataba ambao unaonyesha kuwa amesaliwa na mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba huo .
                     Barcelona's Lionel Messi from Argentina, centre left, scores his goal during a Spanish La Liga soccer match between Real Madrid and FC Barcelona at the Santiago Bernabeu  stadium in Madrid, Spain, Sunday, March 23, 2014. (AP Photo/Andres Kudacki)
Barcelona’s Lionel Messi from Argentina, centre left, scores his goal during a Spanish
 La Liga soccer match between Real Madrid and FC Barcelona at the Santiago
Bernabeu stadium in Madrid, Spain, Sunday, March 23, 2014. (AP Photo/Andres Kudacki)
Ni mwaka mmoja tu umepita tangu Ancelotti alipokuwa anaonekana mfalme ndani ya
Real Madrid baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa mataji mawili msimu uliopita wakati Real ilipotwaa ubingwa wa michuano ya
UEFA wakiwafunga Atletico Madrid kwenye fainali pamoja na kombe la mfalme ambapo waliwafunga Barcelona .
Mapema mwanzoni mwa msimu Real Madrid walionekana kuwa tishio wakati waliposhinda mechi 22 mfululizo kwenye mashindano yote huku wakikamilisha kwa kutwaa ubingwa wa kombe la dunia kwa vilabu .
Hata hivyo mwezi januari mambo yalianza kwenda kombo ambapo Real ilijiuta ikipoteza michezo mfululizo huku ikipoteza uongozi wake wa ligi ya Hispania , kabla ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la mfalme na kukamilisha na dhahma ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa ambapo walifungwa na Juventus .
Newer Post Older Post Home