Takriban
watu 43 wameuawa wakati wa ufyatulianaji wa risasi katika jimbo la
Michoacan nchini mexico kati ya vikosi vya usalama na genge moja lenye
silaha.
Mapigano hayo yalianza wakati magari ya polisi
yalipofyatuliwa risasi kwenye barabara moja kuu katika kijiji kilicho
karibu na mpaka na jimbo la Jalisco.Moja ya megenge hatari zaidi
ya madawa ya kulevya, liko eneo hilo na limekuwa likipigana vita vigumu
katika jimbo la Michoacan kwa miaka mingi.Maafisa kutoka kwa idara za usalama wanaelekelea eneo hilo kufanya uchunguzi.