Maelfu ya Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini wamejitokeza kwa wingi sana kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo jiini Arusha.Mkutano huo ambao lengo lake lilikuwa la kumsikiliza Waziri Mstaafu na pia mbunge wa Monduli,Mh.Edward Ngoyai Lowassa katika kutangaza kwake nia ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu oktoba kwa kupitia chama cha mapinduzi(ccm),aliwasili majira ya saa tisa na kuweza kuhutubia umati wa watu wengi,akieleza kuwa vipaumbele vyake hasa vitakuwa elimu,ubunifu wa ajira kwa vijana,uchumi wa kujitegemea,uboreshaji wa maslahi kwa watumishi wa umma pamoja na mengi kuwaunganisha watanzania bila kujali tofauti zao.
Kwenye mkutano huo Mh Lowassa alikuwa na kauli mbiu ya 'Safari ya matumaini' ambayo ndio imeanza leo,'Nachukia sana umaskini,nataka tuondoe hii hali ya omba omba''narudia tena nataka tuondoe hii hali ya omba omba,ya nchi kuwa tegemezi''Lazima tuwe na maamuzi magumu'narudia tena lazima tuwe na maamuzi magumu'alisema Lowassa.
Mh Lowassa pia aliambatana na viongozi wa chama chake cha Mapinduzi akiwa na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyekitaka chama kumpitisha Lowassa ili safari ya matumaini ianze na kutimizwa akiwataka pia chama kiache tofauti zao na kukaa pamoja kujadili hilo na kusuluhisha.Mzee Kingunge alisema ''Yaliyopita si ndwele tuyagange yajayo''pamoja na kueleza mengi hata kushangazwa na umati mkubwa wa watu ambao amewahi kushuhudia tu kipindi cha Tanu kikidai Uhuru toka kwa wakoloni.




























