Watakaokiuka sheria ya uvutaji sigara mjini Beijing kupigwa faini
Serikali
ya China,imepiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo yote ya wazi
katika mji wa Beijing. Maelfu ya maafisa wameanza kufanya ukaguzi katika
maeneo yote ya wazi na watakaokiuka kufuata sheria hiyo watapigwa
faini.
Hata hivyo China ina wavuta sigara milioni mia tatu wakati
sheria ya kusitisha wavutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa
Beijing ilipopitishwa kwa mara ya kwanza na kushindwa
kutekelezeka.Ripoti inasema kuwa watu wengi wanadhani sheria hiyo ya
kukataza kabisa uvutaji sigara haitafanya kazi.