
Katika Msimu wake wa kwanza tu akiwa na kikosi cha Barca, Enrique alimudu kutwaa makombe matatu baada kubeba Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na juzi kutwaa Kombe la klabu bingwa Ulaya.
Kocha huyu alikataa kueleza kama ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya klabu bigwa ulaya.
Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, ndie alietangaza kuongezewa Mkataba Enrique huo mpya wa kocha huyo.
Enrique, ambae aliwahi kuzichezea Barca na Real Madrid, aliteuliwa Mwaka jana kuwa mbadala wa kocha Tata Martino ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Ajentina.