DK MAGUFULI AONGOZA MAJIMBO MATATU KWENYE MATOKEO YA AWALI.

By | 05:16





By Julius Mathias, Mwananchi
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza matokeo ya awali ya urais kwa majimbo matatu yaliyokamilisha mchakato huo mpaka jana asubuhi.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliyataja majimbo hayo kuwa ni Makunduchi, Paje na Lulindi.
Jaji huyo alisema, Makunduchi lilikuwa na wapigakura 12,742 waliojitokeza ni 10,682 sawa na asilimia 83.83 na hakuna kura zilizoharibika.
Jimboni humo; ACT-Wazalendo imepata 22, ADC 58, CCM 8,406, Chadema 1,769, Chaumma 68, NRA 23 na TLP na UPDP vimepata 18 kila kimoja.
Jimboni Paje kulikuwa na watu 10,276 na waliojitokeza ni 8,326. Kura halali ambazo wagombea husika waligawana zilikuwa 8,047.
ACT ilivuna kura 36, ADC 21, CCM 6,035, Chadema 1,899, Chaumma 28, NRA na TLP nane kila kimmoja na UPDP saba.
Huko Jimbo la Lulindi waliojiandikisha ni 59,027 na walijitokeza ni 45,844 ila kura 1,507 ambazo ni sawa na asilimia 3.29 ziliharibika.
Katika jimbo hilo ACT imepata 528, ADC 362, CCM 31,605, Chadema 11,543, Chaumma 179, NRA na TLP 43 kila kimoja huku UPDP kikivuna kura 34.

Newer Post Older Post Home