MSHINDI ARGENTINA KUAMULIWA DURU YA PILI.

By | 04:16


Scioli MacriImage copyrightAFP
Image captionDaniel Scioli (kushoto) na Mauricio Macri (kulia) watakabiliana kwenye duru ya pili
Wapiga kura nchini Argentina watashiriki duru ya pili ya uchaguzi mwezi ujao baada ya kukosekana kwa mshindi wa moja kwa moja katika duru ya kwanza Jumapili.
Mgombea anayeegemea siasa za mrengo wa kati-kushoto Daniel Scioli aliongoza kwenye kura za mapema, akimpiku mgombea anayeegemea siasa za kati-kulia na ambaye alikuwa meya wa Buenos Aires Mauricio Macri.
Wengi walitarajia Scioli aongoze kwa kura nyingi, lakini hilo halikuwa.
Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika Novemba 22, na itakuwa mara ya kwanza kwa mshindi wa uchaguzi wa urais kupatikana kupitia duru ya pili nchini Argentina.
Baada ya kuhesabiwa kwa 86% ya kura, Scioli alikuwa mbele akiwa na asilimia 35.9%, Bw Macri naye akiwa na 35.2%.
Ili kushinda katika awamu ya kwanza, mgombea alihitaji kushinda 45% ya kura zilizopigwa, au apate angalau asilimia 40% na awe mbele ya mpinzani wa karibu kwa zaidi ya asilimia 10.
"Kilichofanyika leo kitabadilisha siasa za humu nchini," Bw Macri, meya wa Buenos Aires, ameambia wafuasi wake.
Bw Scioli aliteuliwa kugombea urais na rais anayeondoka Cristina Fernandez de Kirchner, ambaye haruhusiwi kuwania baada ya kuhudumu mihula miwili.
Newer Post Older Post Home