HOFU YATANDA EBOLA,NIGERIA.

By | 22:54


Image captionMadaktari wakikabiliana na Ebola
Imeripotiwa taarifa za kuwepo kwa mlipuko mpya wa Ebola katika mji wa Calabar Kaskazini mwa Nigeria.
Shirika la usimamizi wa mambo ya dharura nchini humo linasema kuwa watu kumi wamewekwa kizuizini baada ya kugusana na mtu aliyeonekana kuwa na dalili hizo.Vyombo vya habari nchini humo vinasema mtu huyo alifariki punde baada ya kufikishwa hospitalini.
Sampuli za damu kwa sasa zipo katika majaribio.Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa yake siku ya Jumatano kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na Liberia, zimeweza kuwa na wiki yake ya kwanza bila kuwa na tukio lolote la ugonjwa wa ebola tokea mlipuko wa ugonjwa huo mwezi Machi mwaka 2014. Zaidi ya watu elfu kumi na moja walifariki dunia kwa ugonjwa huo.
Newer Post Older Post Home