Lowassa aliambata na aliyekuwa Waziri mkuu mstaafu katika serikali ya awamu ya tatu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Fredrick Sumaye,pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA),akiwemo muasisi wa Chama hicho mzee Edwin Mtei.
Mh Edward Lowassa alinadi sera zake akizitaja Elimu kuwa kipaumbele kwanza ,elimu kuwa bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu,akiamini wananchi hawawezi kujikomboa kifikra kama hawajawezeshwa kielimu ili kuondoa ujinga na kuleta,maendeleo,kilimo kukiboresha,sekta ya afya kuboreshwa katika ngazi zote za wilaya,kutatua kero ya migogoro ya ardhi,maji,umeme.
Baada ya mkutano huo ambao ulihudhuriwa na maelefu ya wakazi wa Usa river Mh.Edward Ngoyai Lowassa aliweza kuelekea katika viwanja vya sinoni kwa mkutano mwingine wa hadhara.