MAONI YA WATANZANIA WAISHIO NG'AMBO KUHUSU UCHAGUZI.

By | 11:23


Tume ya Uchaguzi
Image captionWatanzania walio nje ya nchi wanafuatilia kwa makini matukio Tanzania
Watanzania walio nje ya nchi hiyo wanafuatilia kwa karibu sana uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Tuliwasiliana na mmoja wao Evarist Chahali ambaye hapa anasimulia jinsi yeye na wenzake wanafuatilia uchaguzi huo na yale wangelipenda yafanyike.
“Wengi wa wana-diaspora wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya uchaguzi mkuu huo kwa sababu, kwanza, kama ilivyo kwa raia wengi wa kigeni wanaoishi nchi za nje, huwa na ukaribu angalau wa kimawasiliano na ndugu, jamaa na marafiki katika nchi zao za asili.
Pili, mazingira ya diaspora, hususan katika nchi zilizoendelea, hamasa ya kutamani kuona nchi zao asili zinapiga hatua kimaendeleo, na uchaguzi mkuu hutoa fursa ya kupata viongozi wapya wanaotarajiwa kuwezesha nchi kusonga mbele.
Tatu, maendeleo ya teknolojia, hasa, matumizi ya teknolojia ya kisasa yanawezesha ufuatiliaji wa matukio mbalimbali nchini Tanzania.
Baadhi Watanzania wanaoishi hapa Uingereza, Marekani, Canada, Denmark na Sweden suala moja lililojitokeza kwa kila mmoja wao ni kutamani kuona Watanzania wote wakinufaika na raslimali za nchi yao.
Suala linalowasikitisha ni sheria inayowanyima wakazi wa diaspora kushiriki katika chaguzi mbalimbali, sambamba na vipingamizi dhidi ya umuhimu wa uraia pacha. Pia wanatamani kuona uchaguzi huo mkuu ukiwa huru na waka haki, na kufanyika kwa amani, na kuwataka wanasiasa wataoshindwa kukubali matokeo. Kadhalika, wanatarajia upande utakaoshinda utafanya jitihada kuwaunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti za kiitikadi.
Kadhalika baadhi wanajadili tatizo la rushwa, na wanaamini ndicho kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa nchi hiyo. Kunao wanaozitaka nchi wahisani kuweka shinikizo zaidi kuhakikisha kuwa misaada wanayotoa inatumika ipasavyo.
Masuala mengine wanayotaka yaangaziwe ni utekelezwaji wa ahadi za wanasiasa ambazo huwa nyingi wakati wa kampeni lakini zinazotekelezwa ni chache, kutilia mkazo sekta za elimu na afya, kushughulikia kero mbalimbali za wananchi kwa nyakati zote na si wakati wa kampeni tu.
Vilevile wengine hawajaridhishwa na mapambano dhidi ya umasikini, sambamba na kuongezeka kwa pengo kati ya matajiri na masikini. Pia baadhi wanaitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania iboreshwe ili kuiongezea serikali mapato yake.
Hayo ni masuala ambayo Watanzania wanaoishi ng’ambo wangependa kuyaona yakitokea Tanzania na wangelipenda sana yapewe kipaumbele na Rais ajaye na serikali yake.”
Newer Post Older Post Home