MAN UNITED,CITY ZAVIMBIANA.

By | 00:27



Kocha wa Man United, Louis Van Gaal akipeana
Kocha wa Man United, Louis Van Gaal akipeana mkono na kocha wa Man City mara baada ya kipenga cha mwisho cha mwamuzi aliyechezesha mechi ya mahasimu hao wa jijini Manchester iliyokwisha kwa matokeo ya 0-0. 

Manchester, England. Timu hasimu za jiji la Manchester, United na Manchester City zimeshindwa kutambiana baada ya kulazimishana sare ya 0-0  katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu England.
Man United  ilikuwa na mchezo mzuri na kuutawala kwa kiasi kikubwa mchezo huo, lakini  ilishindwa kutumia faida hiyo ya kucheza nyumbani kuifunga Man City  iliyonekana kumkosa mshambuliaji wao hatari, Sergio Aguero aliye majeruhi.
Kwa matokeo hayo,  Man City imerudi kileleni mwa  Ligi Kuu  Englandkwa tofauti ya mabao dhidi ya Arsenal iliyoongoza kwa muda baada ya ushindi wao wa juzi wa mabao 2-1 dhidi ya Everton.
Katika michezo mingine iliyochezwa jana, Tottenham  au Spurs iliinyuka Bournemouth kwa mabao 5-1, wakati Sunderland  ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle.
Mechi nyingine ilikuwa baina ya Liverpool na Southampton zilizokuwa zikicheza jana usiku.
Newer Post Older Post Home